1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaIsrael

Netanyahu afanyiwa upasuaji wa kuondoa tezi dume

30 Desemba 2024

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amefanyiwa upasuaji wa kuondolewa kwa tezidume. Upasuaji wa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 75 ulifuatia maambukizi kwenye njia ya mkojo.

https://p.dw.com/p/4ofj6
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Netanyahu anaendelea kupata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa tezi dumePicha: Menahem Kahana/REUTERS

Hospitali inayomtibu Waziri Mkuu huyo imesema yuko katika hali nzuri baada ya shughuli hiyo ya Jumapili. Ilisema anaendelea kupata nafuu katika chumba cha wagonjwa wa kawaida. Mshirika wa karibu wa Netanyahu na Waziri wa Sheria Yariv Levin alipandishwa cheo kwa muda kuwa kaimu waziri mkuu. Upasuaji huo ulisababisha kucheleweshwa kwa kesi ya Netanyahu ya ufisadi wiki ijayo.

Kiongozi huyo wa Israel anashtakiwa kwa udanganyifu, ubadhirifu na rushwa. Katika kikao cha awali Desemba 10, alikanusha madai yote akisema ni ya upuuzi.

Netanyahu, ambaye amekabiliwa na matatizo ya kiafya katika miaka ya karibuni, amejitahidi sana kuimarisha taswira yake kwa umma kuwa yeye ni kiongozi mwenye afya njema na mwenye nguvu. Wakati kukiwa na mengi yanayoendelea katika kanda ya mashariki ya kati inayoshuhudia migogoro, afya ya Netanyahu katika wakati wa vita ni suala linalozusha wasiwasi kwa Waisrael na ulimwengu kwa ujumla.