NEW YORK: Jumuiya ya nchi za kiarabu ina matumaini ya azimio kupitishwa
10 Agosti 2006Kiongozi wa jumuiya ya nchi za kiarabu ana matumaini kwamba azimio la Umoja wa Mataifa juu ya Lebanon huenda lipitishwe juma hili, licha ya tofauti kati ya Marekani na Ufaransa juu ya kuondoka kwa wanajeshi wa Israel kutoka Lebanon.
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, John Bolton, amesema ni vigumu kubashiri matokeo ya mazungumzo yanayoendelea lakini kuna matumaini ya kufikia muafaka.
Waziri mkuu wa Lebanon, Fuad Siniora, amesema mpaka sasa hakuna ufanisi wowote uliopatikana katika juhudi za baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio linalonuia kumaliza mapigano kati ya Israel na kundi la Hezbollah.
Baada ya kukutana na naibu waziri wa mambo ya ndani wa Marekani, David Welch, mjini Beirut, Siniora amesema hatajarii lolote kufanyika katika siku chache zijazo.