Niger yazindua kampeni ya chanjo dhidi ya Malaria
21 Septemba 2024Waziri wa afya Garba Hakimi amesema wamezindua kampeni kubwa ya chanjo huku awamu ya kwanza ikifanyika Alhamisi katika mji wa Kusini Magharibi wa Gaya, kitovu cha ugonjwa wa malaria unaoenezwa na mbu.
Kwa wastani wagonjwa wa malaria milioni tano hurekodiwa nchini Niger kila mwaka huku zaidi ya watu 5,000 wakipoteza maisha.
Soma pia: Dola bilioni moja zaahidiwa kuwezesha uzalishaji wa chanjo Afrika
Kulingana na takwimu za shirika la afya duniani WHO, mnamo mwaka 2022, malaria ilisababisha vifo vya zaidi ya watu 600,000 duniani kote – asilimia 95 kati yao wakiwa barani Afrika na asilimia 80 wakiwa Watoto chini ya umri wa miaka mitano.
WHO imesema katika taarifa kuwa dawa ya kupambana na malaria RTS,S – iliyotengenezwa na kampuni ya dawa ya Uingereza ya GSK – itatumika kwenye kampeni hiyo ya chanjo nchini Niger ambayo iliidhinisha mwaka 2022.