Njaa yauwa watoto 29 Malawi
27 Septemba 2005Matangazo
Lilongwe:
Uhaba wa chakula katika eneo la kusini mwa Afrika, umesababisha vifo vya watoto 29 katika kituo kimoja cha kuwalea watoto nchini Malawi, moja wapo ya nchi zilizoathirika vibaya . Shirika la mpango wa chakula la umoja wa mataifa, linasema zaidi ya watu milioni 10 wanahitaji msaada katika kanda hiyo, kwa sababu ya mavuno mabaya ya mahindi-chakula cha msingi katika nchi nyingi za kusini mwa Afrika. Shirika la msaada la Uingereza –OXFAM, linasema ulimwengu lazima uchukue hatua, au muda si mrefu eneo hilo la kusini mwa Afrika linaweza kukumbwa na janga la njaa sawa na lile lililotokea nchini Niger.