1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Njia zaidi za kiutu zaundwa Ukraine

Hawa Bihoga
14 Aprili 2022

njia tisa za kupitisha misaada ya kiutu zimeundwa Ukraine katika mikoa ya Luhansk na Donesk ili kuwawezesha wananchi kuondoka katika miji iliyozingirwa na vikosi vya Urusi kwenye maeneo hayo.

https://p.dw.com/p/49wSn
Ukraine Waffensystem Carl Gustaf M4
Picha: Andrew Marienko/AP Photo/picture alliance

Wakati hali ikiendelea kuzorota katika miji iliyoshambuliwa vibaya nchini Ukraine, njia tisa za kupitisha misaada ya kiutu zimewekwa leo Alkhamisi katika mikoa ya Luhansk na Donesk ili kuwawezesha wananchi kuondoka katika miji iliyozingirwa katika maeneo hayo. 

Mzozo huo ambao umeendelea kuchukua sura tofauti kila kukicha leo umeingia siku ya hamsini, huku maelfu ya watu wakiripotiwa kuuwawa, zaidi ya milioni kumi wakilikimbia taifa hilo, RaisVolodmiry Zelensky akiwa mstariwa mbele katika kuhamasisha raia katika kulitetea taifa lao huku akitafuta uungwaji mkono wa kimataifa katika kukabiliana na vikosi vya Urusi.

Ikiwa ni sehemu ya kuendelea kuokoa mamia ya raia waliokwama katika miji iliyozingirwa na majeshi ya Urusi, mikoa ya Luhansk na Donetsk imetangazwa na mamalaka za Ukraine kuwa itatumika kama njia salama za kiutu ili kuwawezesha raia kuondoka katika maeneo hayo.

Soma zaidi:Vikosi vya Urusi vinazidi kusonga mbele mjini Mariupol

Moja kati ya njia hizo tisa imeundwa kwa ajili ya magari ya binafsi.

Hata hivyo, Naibu Waziri Mkuu wa Ukraine,  Iryna Vereshchuk, amesema kwamba njia hizo zitafanya kazi kama ilivyokusudiwa endapo Urusi itasitisha mashambulizi katika maeneo hayo.

 Alisema treni ya kuwahamisha raia kutoka mji wa Pokrovsk itawapeleka raia kwanza Kiev kabla ya kuendelea Chop kusini ulio magharibi mwa Ukraine.

 

Katikati ya mzozo Meli ya kijeshi ya Urusi yambambuliwa

Meli moja ya kivita ya Urusi imeharibiwa vibaya na wanajeshi wake kuokolewa kutoka kwenye meli hiyo kufuatzia mripuko ambao umesababishwa na makombora ya Ukraine. 

Russland Kreuzer Moskva
Meli ya kivita ya Urusi MoskvaPicha: Alexey Pavlishak/REUTERS

Kuharibiwa kwa meli hiyo ya kivita ya enzi za Kisovieti inayoitwa Moskuva itakuwa ni hasara kubwa kwa Urusi, baada ya siku 50 ya vita hivyo, wakati ambapo Urusi inajiandaa kwa mashambulizi mapya katika eneo la mashariki la Donbas, ambayo yataonesha muelekeo wa vita hivyo.

Soma zaidi:Urusi yazidisha mashambulizi katika miji ya Ukraine

Mbali na kushambuliwa kwa meli hiyo ya kivita, jeshi la Urusi limetangaza leo Alkhamisi kuwa limechukua udhibiti kamili wa bandari ya Mariupol iliyoharibiwa kwa kiasi kikubwa. 

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Urusi Igor Konashenkov alisema wanajeshi waliobaki wa Ukraine katika jiji wamezuiliwa  na  hawawezi kutoroka. 

Lakini meya wa jiji la Mariupol lililokumbwa na mzozo mkubwa, Vadym Boichenko, aliliambia shirika la utangazaji la Ujerumani, ARD, kwamba Mariupol ipo chini ya udhibiti wa Ukraine.

 Aliita taarifa ya Urusi kuchukua udhibiti wa bandari ya Mariupol ni na zaidi ya wapiganaji 1000 wa ukraine kujisalimisha ni uongo. Mji huo umekuwa chini ya mzingiro wa vikosi vya Urusi na wale wanaounga mkoni vikosi vya Urusi.

 

Chanzo:Mashirika