1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nkurunziza azikwa nchini Burundi

26 Juni 2020

Aliyekuwa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza leo ndipo ameziwa katika kijiji cha  Munsinzira kwenye mkoa wa Gitega katikati mwa Burundi.

https://p.dw.com/p/3ePId
Präsident Burundis Pierre Nkurunziza
Picha: Reuters/C. Guy Siboniyo

Mjane wak, Denise Nkurunziza amesema kifo cha mume wake ni matakwa yake Mungu na amemuomba aendelee kuwalinda na kuendeleza urithi wake. Amida ISSA na taarifa kamili. Katika kipindi cha majira ya saa 9 na nusu ndipo mwili wa rais Pierre Nkurunziza ulizikwa katika kaburi maalum huko Gitega na kusindikizwa na majenerali 10 wa  jeshi na kuhudhuriwa na mkewe pamoja na watoto wake watano.

Baada ya kuzikwa jeshi lilifyatua mizinga 21 kama heshima za mwisho kwa hayati rais Nkurunziza ambaye pia alikuwa mwanajeshi.
Mwili wa Nkurunziza ulisafirishwa kwa ndege kutoka kwenye hospitali ya Karusi alikofia hadi kwenye uwanja wa michezo wa Ingoma mjini Gitega alikopewa heshima za mwisho  na raia na wote waliohudhuria mazishi yake.

Maombi ya viongozi wa dini

Viongozi wa dini tatu kuu nchini Katoliki, Protestanti na Waislamu wote walimuomba Mungu ampokee na kumpa makaazi mema.
Mjane wake bi Denise Nkurunziza ametowa hotuba ya kusisimuwa alipobainisha kuwa kifo chake ni matakwa yake Mungu, aliyempa pia yeye na wanaye nguvu na ujasiri wa kukubali. ''Muumba ni wewe mwenye nguvu, ni wewe unayefisha tunakuomba Mwenyezi Mungu kujalia kupatikana wengine watakaokuwa kama Nkurunziza na mimi na  wanetu tutaendeleza uridhi wa hayati''.

Burundi Agathon Rwasa kondoliert zum Tod von Pierre Nkurunziza
Picha: DW/Antéditeste Niragira


Baada ya mwili kuingizwa kaburini katika shughuli iliyofanyika kwa faragha yaliwekwa mashada ya mauwa ambapo wameanza wanaye na kufuatiwa na Rais Evariste Ndayishimiye, nachama chake Cndd Fdd.

Baada ya kuzikwa kwake rais huyo wa zamani wa Burundi, baadhi ya raia wamekuwa na maoni tafauti kama kumbukumbu ya rais Pierre Nkurunziza.''Alifanya kazi nzuri 2005 hadi 2015. Lakini baada ya hapo aliharibu kila kitu kwani alikalia muhula kinyume cha sheria, maisha yamekuwa magumu sana hasa kwa wafanyakazi wa serikali''. Mazishi ya Pierre Nkurunziza yameudhuriwa pia rasi mstaafu wa Tanzania, Jakaya Mrisho kikwete. Zambia imewakilishwa na mke wa rais. Mabalozi wa nchi mbalimbali pamoja na maafisa wa mashirika ya kimataifa pia wamehudhuria mazishi hayo.