Norway kuchukua jukumu la ulinzi wa anga wa Poland
3 Desemba 2024Matangazo
Nchi hiyo itapeleka kikosi chake cha wanajeshi 100, mifumo ya ulinzi wa anga pamoja na ndege za kivita chapa F-35 kusimamia ulinzi.
Hayo yametangazwa na waziri wa ulinzi wa Norway Bjorn Arild Gram, ambaye pia amefafanuwa kwamba uwanja huo wa ndege wa Poland ni muhimu kwa usafirishaji wa vifaa vya kijeshi na pia shughuli za usafirishaji wa dharura wa wanaohitaji huduma za matibabu, zinazosimamiwa na Norway.
Kwa mujibu wa Norway mifumo ya ulinzi, wanajeshi na ndege za kivita zitapelekwa katika kipindi cha siku kadhaa zijazo na ujumbe huo wa Norway utaendesha shughuli zake hadi msimu wa Pasaka.