OSLO : Mchumi wa Bangladesh apokea Tuzo ya Nobel
10 Desemba 2006Matangazo
Mchumi wa Bangladesh Muhammad Yunus amepokea Tuzo ya Amani ya Nobel katika seherehe iliofanyika kwenye mji mkuu wa Oslo.
Katika hotuba yake ya kukubali tuzo hiyo Yunus amewataka viongozi duniani kuendelea kupiga vita umaskini badala ya kutumia mabilioni ya fedha katika vita kama vile vilioko hivi sasa nchini Iraq. Amesema umaskini,kukosekana kwa haki za binaadamu na dhuluma za kijamii ni mambo yanayotishia sana amani duniani.
Yunus ni muasisi wa Benki ya Grameen ambayo imesaidia kuwatowa kwenye umaskini mamilioni ya watu kwa kuwapatia mikopo midogo midogo wale wasiostahili kupatiwa mikopo na benki za kawaida.