1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMamlaka ya Palestina

Oxfam yatahadharisha juu ya hali mbaya ya kibinadamu Gaza

23 Desemba 2024

Oxfam imesema malori 12 pekee ndiyo yaliyosambaza chakula na maji kaskazini mwa Gaza katika kipindi cha miezi miwili na nusu na kutahadharisha juu ya hali mbaya zaidi ya kibinadamu katika eneo hilo lililozingirwa.

https://p.dw.com/p/4oUZG
Khan Yunis | Shule | Gaza
Wapalestina waliofurushwa makwao wakitazama uharibifu uliofanyika baada ya shambulio la anga la Israel dhidi ya shule iliyogeuzwa makaazi eneo la Khan Yunis.Picha: Hani Alshaer/Anadolu/picture alliance

Oxfam imeeleza katika taarifa kuwa ucheleweshaji wa makusudi na vizuizi vya kimfumo vilivyowekwa na jeshi la Israel vimesababisha malori 12 pekee kuwasilisha misaada kwa Wapalestina wanaokabiliwa na njaa.

Katika ripoti iliyoangazia hali ya upatikanaji wa maji, shirika la haki za binadamu lenye makao yake mjini New York la Human Rights Watch, mnamo siku ya Alhamisi limesema kile ilichokiita juhudi za makusudi za mamlaka ya Israel kuwanyima maji wakaazi wa Gaza, hali ambayo imesababisha vifo vya maelfu ya watu.

Soma pia:  Papa Francis azungumzia tena "ukatili" wa Israel huko Gaza

Israel ambayo imeweka vizuizi vikali katika njia za kuingia ukanda wa Gaza tangu kuanza kwa vita, mara nyingi imekuwa ikilaumu kile inachosema ni kushindwa kwa mashirika ya misaada kuratibu na kusambaa misaada mikubwa.

Tuhuma hizo ni za hivi karibuni dhidi ya Israel – na kukanushwa na mamlaka za nchi hiyo katika vita vyake vya miezi 14 dhidi ya kundi la Hamas.