PANAMA CITY: Wapanama kuamua ikiwa mfereji upanuliwe
22 Oktoba 2006Matangazo
Wapiga kura nchini Panama leo Jumapili wanapiga kura ya maoni kuhusu mpango wa serikali wa kutaka kupanua mfereji wa Panama.Uchunguzi wa maoni unaonyesha kuwa mradi huo utakaogharimu Dola bilioni 5 utapata kura za kutosha.Lakini wapinzani wa mradi huo waliandamana siku ya Ijumaa wakisema mradi huo utazidisha deni kubwa la nchi hiyo.Serikali lakini inasema,mfereji huo uliofunguliwa mwaka 1914,lazima upanuliwe na uongezwe kina,ili meli za mizigo za kisasa,ziweze kupitia njia hiyo wakati ambapo uchumi duniani unapanuka.