Papa asikitishwa na vifo vya wafanyakazi wa misaada Gaza
3 Aprili 2024Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis leo ameelezea kusikitishwa kwake na vifo vya wafanyakazi saba wa mashirika ya kutoa misaadawaliouwawa na mashambulizi ya Israel, walipokuwa katika harakati za kuwasilisha misaada huko Gaza.
Akizungumza wakati wa hotuba yake ya kila wiki Baba Matakatifu mwenye umri wa miaka 87 amesema, anaziombea familia za wafanyakazi hao na kutoa wito wa njia za uwasilishwaji misaada kwa watu wa Gaza kufunguliwa na kuachiwa kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas.Marekani, Uingereza na EU zalaani mauaji kwa watoa misaada
Wito huu wa Papa Francis unakuja wakati ambapo Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk amesema leo kuwa, shambulizi hilo la Israel limevuruga mahusiano ya nchi hizo mbili na kwamba Israel inauweka uungaji mkono wa Poland kwake katika mtihani mkubwa.
Haya yanafanyika wakati ambapo wizara ya afya ya gaza inayoendeshwa na kundi la Hamas, imesema kufikia sasa Wapalestina karibu 33,000 wameuwawa kutokana na mashambulizi ya Israel.