1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa atoa wito wa kunyamazishwa kwa silaha

26 Desemba 2024

Papa Francis alitumia hotuba yake kutoa wito wa amani ya haki nchini Ukraine, kusitisha vita Gaza na kuachiwa kwa mateka wa Kiisrael.

https://p.dw.com/p/4oZwv
Vatikan I Papa Francis
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis akiongoza misa mjini Vatican.Picha: Alberto Pizzoli/AFP

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, ametoa wito wa "silaha kunyamazishwa" duniani katika hotuba yake ya Krismasi, akihimiza amani Mashariki ya Kati, Ukraine, na Sudan huku akilaani hali mbaya ya kibinadamu Gaza.

Akizungumza katika Uwanja wa Kanisa la Mtakatifu Petro, Papa alihimiza mazungumzo ya amani Ukraine, kusitisha mapigano Gaza, na kuachiliwa mateka wa Israeli. Pia alitoa wito wa msaada kwa waathirika wa vita na njaa Sudan.

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, alilaani mashambulizi ya Urusi ya Krismasi dhidi ya miundombinu ya umeme, huku Urusi ikiripoti vifo vya watu watano kutokana na mashambulizi ya Ukraine.