Papa Francis awasili Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo
31 Januari 2023Matangazo
KINSHASA:
Papa Francis anazuru taifa hilo kubwa ya Afrika ya Kati, lenye utajiri mkubwa wa madini lakini ambako mamilioni ya watu wamepoteza makazi na wanaishi katika umaskini. Francis ndiyo papa wa kwanza kuitembelea Kongo tangu John Paul II mnamo mwaka 1985, wakati huo ikiitwa bado Zaire. Karibu nusu ya raia milioni 90 wa Kongo ni waumini wa Kikatoliki. Baada ya hafla ya kumkaribisha papa na mkutano na rais Felix Tshisekedi, kiogozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani atato hotuba kwa viongozi wa serikali, wanadiplomasia na wawakilishi wa mashirika ya kiraia. Kesho Jumatano ataongoza misa na kukutana na waathirika wa vurugu kutoka eneo la mashariki mwa Kongo, linalozongwa na mapigano kati ya waasi na wa kundi la M23 na vikosi vya serikali.