1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan Kusini

Papa: Makanisa yapaze sauti dhidi ya dhuluma Sudan Kusini

4 Februari 2023

Papa Francis amesema kuwa makanisa nchini Sudan Kusini lazima yapaze sauti zao dhidi ya dhuluma na matumizi mabaya ya madaraka. Anafanya ziara katika taifa hilo changa duniani

https://p.dw.com/p/4N68C
Südsudan Juba Besuch von Papst Franziskus | Treffen mit Jesuiten
Picha: VATICAN MEDIA/REUTERS

Katika siku yake ya pili nchini Sudan Kusini, Kiongozi huyo wa kanisa katoliki amewahutubia maaskofu wa Kikatoliki, mapadre na watawa katika mji mkuu Juba wakati Askofu Mkuu wa Kanisa la Uingereza na kiongozi wa Kanisa la Scotland wakiendesha ibada katika maeneo mengine.

Papa Francis amesema kama viongozi wa kanisa, nao pia wanatakiwa kuwaombea watu, kupaza sauti zao dhidi ya dhuluma na matumizi mabaya ya madaraka ambayo yanakandamiza na kutumia vurugu ili kukidhi malengo yao. Papa Francis, Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Welby na Mkuu wa Kanisa la Scotland Iain Greenshields watakutana na watu waliopoteza makazi kutokana na vita na kusikiliza simulizi zao baadae leo.