1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUjerumani

Pato la taifa Ujerumani kunywea hadi asilimia 0.5 mwaka 2023

29 Agosti 2023

Taasisi ya uchumi ya Ujerumani imesema pato jumla la nchi hiyo, ambayo ni injini ya uchumi barani Ulaya, linatarajiwa kupungua hadi kwa asilimia 0.5 mnamo mwaka huu.

https://p.dw.com/p/4VhIj
Taasisi ya uchumi ya Ujerumani imeeleza kuwa, uchumi wa nchi umeathirika hasa kutokana na migogoro iliyosababishwa na siasa za kikanda.
Taasisi ya uchumi ya Ujerumani imeeleza kuwa, uchumi wa nchi umeathirika hasa kutokana na migogoro iliyosababishwa na siasa za kikanda.Picha: Steinach/imago images

Takwimu hizo zinabainisha kwamba Ujerumani imeshaingia katika mdodoro wa uchumi.

Katika ripoti yake, taasisi ya uchumi ya Ujerumani imeeleza kuwa, uchumi wa nchi umeathirika hasa kutokana na migogoro iliyosababishwa na siasa za kikanda, ikiwa pamoja na vita vya nchini Ukraine na mivutano na China.

Hali hiyo itasababisha ukosefu wa ajira kwa kiwango cha asilimia 5.5.

Licha ya kiwango cha mfumuko wa bei kupungua kidogo, kwenye eneo la nchi zinazotumia sarafu ya Euro,viwango vya juu vya riba vitatatiza ununuzi wa mahitaji kwa watu nchini na pia vitatatiza uekezaji vitega uchumi.