PKK-Pipa la baruti
7 Oktoba 2008Chama cha waasi cha wakurdi nchini Uturuki PKK kwa mara nyengine tena kimeonesha nguvu zake za kijeshi hivi punde kilipofanya hujuma mbali mbali mpakamni mwa Uturuki na Irak na kuwaua wanajeshi 15 wa kituruki .Uturuki inabainika iko mbali kupata ufumbuzi wa tatizo la wakurdi.Haitakua busara kwahivyo, kwa Uturuki sasa kuchukua hatua ya kukipiga marufuku chama cha wakurdi cha DTP.
Juhudi zote zilizofanywa na wajumbe wa serikali ya Uturuki miaka iliopita kuutatua mgogoro wa wakurdi zilikua bure.Pipa la baruti -chama cha wakurdi cha PKK-bado linafuka moto.Tangu katika nchi za ulaya hata nchini Uturuki kwenyewe,mapambano ya silkaha kati ya jeshi la uturuki na wapiganaji wa PKK yamesababisha vifo 10.
Na ijumaa iliopita wanajeshi 15 wa kituruki waliuliwa katika hujuma iliofanywa na wapiganji wa PKK katika kituo chao milimani .PKK ilipoteza wapiganaji 20 katika hujuma hiyo.
Kwa mara nyengine hasira zilielezwa juu ya tokeo hilo tangu na serikali ya Ujerumani mjini Berlin hata Umoja wa ulaya mjini Brussels na hata huko Washington,Marekani.Isitoshe, kila kukicha watu wanauwawa wakiwa ama wamevaa mavazi ya kijeshi ya vikosi vya ulinzi vya Uturuki au ya PKK.
Hujuma ya hivi punde imezusha ghadhabu kubwa na uzalendo nchini kote Uturuki.Hasa hii inabainika katika viwanja vya mpira vya Uturuki.
Huzuni na hasira za wananchi wa uturuki zinalengwa pia dhidi ya uongozi wao na jeshji lao.Wanauliza:kwanini vituo vya m pakani havilindwi sawa sawa.Kituo cha mpakani cha Aktutun mkoani Hakkari,kimekuwa kikihujumiwa mara kwa mara hivi karibuni na wanamgambo wa PKK.
Serikali ya Uturuki tayari mnamo miaka ya 80 na 90 ilishindwa kulipatia ufumbuzi tatizo la wakurdi.Kwa upande mmoja, imekuwa ikilieleza tatizo la wakurdi si lolote ,si chochote, bali ni "gengi la magaidi" na mara nyingi ikisema, kundi la PKK na hasa baada ya kutiwa mbaroni kwa kiongozi wake Abdullah Ocalan,limeshazikwa na kushindwa vita.
Kwa upande wapili, serikali ya Uturuki katika kupambana na PKK ikitumia hata silaha isiokubalika ya mateso.halafu ikikandamiza uhuru wa kujieleza na kuwatilia shaka wakurdi wote-jumla,jamala kwamba ni chungu kimoja na wapiganaji wa PKK.Hakujakuwa na mpango wa kujenga imani ya wakurdi katika dola la Uturuki.
Wanasiasa wa Umoja wa Ulaya ,yafaa sasa kuacha desturi ya kukiangalia chama cha PKK sio tu cha kigaidi karatasini , bali pia kukichukulia hatua zinazostahiku kupambana na chama cha kigaidi.PKK hakiwakilishi umma wote wa wakurdi nchini Uturuki na si muakilishi wao kisiasa.
Bunge la Uturuki mjini Ankara, linapanga kesho kwa wingi mkubwa kulipa jukumu jeshi kupambana vikali zaidi mpakani na Irak na PKK.Ni chama cha wakurdi cha DTP ndicho pekee kitakachopaza sauti kupinga mpango huo.Itakua kosa kubwa kukipiga marufuku DTP.PKK ndio itakayo nufaika na hatua kama hiyo.