1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Poland inaadhimisha miaka 85 tangu Vita vya Pili vya Dunia

1 Septemba 2024

Poland leo imeadhimisha miaka 85 tangu kuzuka kwa Vita vya Dunia kwa hafla ya kila mwaka ya ukumbusho iliyofanyika alfajiri kwa kukumbuka mashambulio ya kwanza ya Ujerumani ya Manazi ambayo yalisababisha mzozo huo mbaya.

https://p.dw.com/p/4k9Bz
Shambulio la Poland Septemba 1939
Wanajeshi wa Ujerumani wakibomoa kizuizi kwenye mpaka wa Ujerumani na Poland, katika eneo ambalo halijafahamika hadi sasa.Picha: AP/picture alliance

Takriban wapoland milioni 6 waliuwawa katika vita hivyo vilivyouwa jumla ya watu milioni 50 wakiwemo wayahudi milioni 6,wengi raia wa Poland, katika kile kinachoitwa Holocaust. Akizungumza katika eneo la pwani ya Baltic, la Westerplatte nchini Poland ,zilikofanyika kumbukumbu hizo, waziri mkuu wa nchi hiyo Donald Tusk amesema funzo la vita vya pili vya dunia halijasahaulika.

Kiongozi huyo wa Poland pia amefananisha kilichotokea wakati huo na kinachotokea sasa katika nchi jirani ya Ukraine akisema vita hivyo vinarudi tena kutokea upande wa Mashariki. Amezitolea mwito nchi wanachama wa jumuiya ya NATO kujitoa kikamilifu kiulinzi dhidi ya uchokozi unaoshuhudiwa hivi sasa katika uwanja wa vita nchini Ukraine.