1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi Kenya yatumia nguvu kuzuwia maandamano dhidi ya kodi

7 Julai 2023

Polisi ya Kenya leo imefyatua mabomu ya kutoa machozi leo kuwatawanya waandamanaji wanaopinga sheria mpya ya fedha iliyoongeza maradufu kodi ya nishati na kuanzisha tozo mpya ya nyumba kwa waajiriwa.

https://p.dw.com/p/4TZU5
Kenia Kenianische Aktivisten demonstrieren in Nairobi gegen ein unpopuläres Finanzgesetz
Picha: Thomas Mukoya/REUTERS

Picha zilizorushwa kwenye kituo kimoja cha televisheni nchini humo zimewaonyesha waendesha magari wakijaribu kuyageuza magari yao na kurudi walikotoka, huku waandamanaji wakikimbia, wakati polisi walipofyatua mabomu hayo katika mji wa bandari wa Mombasa.

Kulikuwa na ufyatuaji zaidi wa mabomu hayo ya kutoa machozi mjini Nairobi wakati waandamanaji walipofunga sehemu ya barabara katika mji huo.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga ameitisha maandamano hayo kupinga ongezeko la kodi, ambalo limeanza kutekelezwa licha ya amri ya mahakama kusitisha hatua hiyo.