1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGeorgia

Polisi nchini Georgia yawakamata waandamanaji 107

30 Novemba 2024

Polisi nchini Georgia imeripoti kuwakamata watu 107 walioshiriki maandamano usiku wa jana katika mji mkuu pekee wa Tbilisi.

https://p.dw.com/p/4nbMY
Waandamanaji katika mji wa Tbilisi
Waandamanaji nchini Georgia wakipambana na polisi. Waandamanaji hao wanaipinga serikali kwa kusitisha majadiliano ya kujiunga na Umoja wa UlayaPicha: Irakli Gedenidze/REUTERS

Waandamanaji hao waliwarushia mawe polisi, kuweka vizuizi na kuchoma vitu, hii ikiwa ni kulingana na taarifa ya polisi.

Idadi hiyo ya waandamanaji waliokamatwa inatajwa kuwa kubwa zaidi katika wiki za karibuni kufuatia ushindi unaozozaniwa wa chama tawala cha Georgian Dream, kwenye uchaguzi wa bunge wa mwezi Oktoba.

Waandamanaji hao waliokusanyika nje ya bunge la Georgia kwa usiku wa pili mfululizo jana Ijumaa, wanapinga uamuzi wa serikali kusitisha mazungumzo ya kujiunga na Umoja wa Ulaya