Polisi Pakistan yatoa mashtaka mapya dhidi ya Imran Khan
29 Novemba 2024Matangazo
Polisi nchini Pakistani imefungua mashtaka kadhaa dhidi ya waziri mkuu wa zamani Imran Khan, mkewe Bushra Bibi, na wengine kwa kuchochea vurugu, baada ya siku kadhaa za maandamano yaliyosababisha vifo vya watu sita.
Bushra Bibi aliongoza maelfu ya watu kudai kuachiliwa kwa Khan, ambaye yuko gerezani tangu Agosti 2023. Polisi waliwakamata takriban waandamanaji 1,000, na mashtaka yamewasilishwa dhidi ya Khan na Bibi kwa kuvuruga amani.
Soma pia: Imran Khan ahukumiwa kwenda jela miaka 10
Serikali inadai kuwa waandamanaji walikuwa na silaha na kulenga kuchukua mji mkuu. Mwandishi habari wa Pakistan Matiullah Jan, anaechunguza ukandamizaji wa vikosi vya usalama dhidi ya waandamanaji, amekamatwa pia na kufunguliwa mashtaka ya ugaidi.