Polisi Uganda yatishia Waandishi
16 Mei 2013Polisi nchini Uganda imetishia kuwafungulia mashitaka mhariri na waandishi wawili wa gazeti la kibinafsi la Daily Monitor, kuhusiana na barua iliyochapishwa na gazeti hilo juu ya kile kinachojulikana nchini Humo kama Mradi wa kumtayarisha mwana wa rais Yoweri Museveni, Brigedia Muhozi, kukirithi kiti cha baba yake. Barua hiyo iliandikwa na mkuu wa kitengo cha upelelezi cha Uganda Jeneral David Sejusa, akidai kuwa kuna mpango wa kuwauwa maafisa wanaoupinga mpango huo. Kuhojiwa kwa waandishi hao kumepingwa na wenzao nchini Uganda, ambao wanakuchukulia kama kitisho kwa uhuru wao. Kusikiliza zaidi kuhusiano na mkasa huo sikiliza mahojiano ya Daniel Gakuba na Ali Mutasa, mwandishi wa habari aliyeko nchini Uganda kwa kubonyeza alama ya kusikilizia masikioni hapo chini.
Mwandishi: Daniel Gakuba
Mhariri: Abdul-Rahman