Polisi Ujerumani yavunjwa soko haramu la mtandaoni
12 Januari 2021Katika wakati wa kufungwa kwake, soko hilo la siri la mtandaoni lilikuwa na watumiaji karibu 500,000 na zaidi ya wauzaji 2,400 kutoka kote duniani, wakati ambapo janga la virusi vya corona limepelekea sehemu kubwa ya biashara ya madawa mitaani kuhamia mtandaoni.
Waedesha mashtaka wamesema polisi katika mji wa kaskazini wa Oldenburg walifanyikiwa kumkamata mtu anaedaiwa kuwa mwendeshaji wa mtandao huo mwishoni mwa wiki.
Taarifa imeongeza kuwa wachunguzi waliweza pia kulifunga soko na kuzima server yake siku ya Jumatatu, wakiitaja hatua hiyo kuwa hitimisho la operesheni ya kimataifa iliyodumu kw amiezi kadhaa.
Jumlya ya miamala isiopungua 320,000 ilifanyika kupitia soko hilo haramu la mtandoani, ikiwemo miamala zaidi ya 4,650 ya sarafu za mtandaoni maarufu bitcoin na 12,800 ya monero - ambazo ni sarafu mbili miongoni mwa sarafu maarufu zaidi za mtandaoni zinazouzwa sana.
soma pia: Kompyuta na Mtandao wa Internet –Kipindi 2 – Kununua kompyuta
Kwa viwango vya sasa vya ubadilishaji fedha, miamala hiyo iliwakilisha biashara yenye thamani ya euro milioni 140, sawa na dola la Marekani milioni 170.
Biashara zinazofanyika darknet
Mtandao huo ulitoa huduma za mauzo ya kila aina ya madawa ya kulevya, pamoja na pesa bandia, data bandia na zilizoibwa za kadi za fedha, simukadi za siri, programu za udukuzi na mambo mengine mengi tu.
Raia wa Australia mwenye umri wa miaka 34 anaeaminika kuwa mwendeshaji wa mtandao huo wa DarkMarket, alikamatwa karibu na mpaka wa Ujerumani na Denmark, mara baada ya kukamatwa kwa server zaidi ya 20 zilizokuwa zinatumika nchini Moldova na Ukraine.
Wachunguzi wanatazamia kutumia data zilizohifadhiwa katika server hizo kuanzisha uchunguzi mpya dhidi ya waongozaji, wauzaji na wanunuzi kwenye soko hilo la siri la mtandaoni. Mshukiwa mkuu alifikishwa mbele ya jaji lakini alikataa kuzungumza.
Soma pia: Sheria ya makosa ya mtandao yaanza Tanzania
Kitendo cha usimamizi wa sheria ya madawa katika idara ya upelelezi wa ndani nchini Marekani, FBI, na mamlaka ya kodi IRS, zilishiriki katika uchunguzi huo pamoja na polisi kutoka Australia, Uingereza, Denmark, Uswisi, Ukraine na Moldova, huku shirika la polisi barani Ulaya Europol, likitekeleza jukumu la uratibu wa operesheni nzima.
Mtandao wa siri wa darknet, unahusisha tovuti ambazo zinaweza kuingiwa tu kwa kutumia programu au idhini makhsusi, na hivyo kuhakikisha usiri wa watumiaji.
Chanzo: AFPE