1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi wa Kenya wakabiliana na waandamanaji

2 Mei 2023

Polisi nchini Kenya wamekabiliana katika mji mkuu Nairobi na waandamanaji wanaoipinga serikali katika duru nyingine mpya ya maandamano yaliyoitishwa na kiongozi wa upinzani, Raila Odinga.

https://p.dw.com/p/4Qo2o
Waandamanaji wakiwa wamechoma lori katika barabara ya Ngong, jijini Nairobi.
Kumekuwa na maandamano ya hivi karibuni nchini Kenya ya wafuasi wa upinzani wanaodai mabadiliko dhidi ya hali mbaya nchini humo.Picha: Ben Curtis/dpa/picture alliance

Waandamanaji waliojitokeza kuanzia asubuhi waliweka vizuizi kwenye barabara kuu kadhaa katika mji wa Nairobi huku wakiwarushia mawe polisi. Maafisa wa Polisi walitumia mabomu ya kutowa machozi dhidi ya waandamanaji hao.

Ripoti pia zimeeleza kwamba basi moja limeteketezwa. Aidha maandamano pia yameshuhudiwa katika mji wa Kisumu ambako shughuli za kibiashara zimesimama,wakati polisi wakikabiliana na waandamanaji.

Kisumu ni ngome kuu ya kambi ya upinzani nchini Kenya. Upinzani unaoongozwa na Raila Odinga unataka hatua zichukiliwe kudhibiti gharama za maisha na yafanyike mageuzi katika tume ya uchaguzi iliyosimamia uchaguzi uliopita uliomuingiza madarakani rais William Ruto.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW