1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi ya Kenya yasema zaidi ya watu 238 wamekamatwa

21 Machi 2023

Polisi nchini Kenya imesema,watu 238 wamekamatwa nchi nzima, wakati wa maandamano yaliyosababisha vurugu hapo jana.

https://p.dw.com/p/4P12J
Proteste in Kenia
Picha: Ben Curtis/AP/dpa/picture alliance

Mkuu wa jeshi la polisi Japhet koome kupitia taarifa amesema watu 213 walikamatwa katika jiji la Nairobi  na polisi 24 walijeruhiwa. Maandamano hayo yaliofanyika kupinga ongezeko la gharama za maisha nchini humo, yalisababisha maafisa 31 wa polisi kujeruhiwa.

Polisi walitumia mabomu ya kutowa machozi na mabomba ya maji dhidi ya waandamanaji ambao baadhi walikuwa wakirusha mawe na kuchoma moto matairi. Polisi pia walifyetua mabomu ya kutowa machozi dhidi ya msafara wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga aliyeitisha maandamano hayo nchi nzima.

Soma pia: Mwanafunzi auawa wakati upinzani Kenya ukifanya maandamano

Machafuko yaliyoshuhudiwa jana nchini Kenya yalikuwa mabaya zaidi kuwahi kuonekana tangu alipoingia madarakani William Ruto miezi sita iliyopita baada ya kumshinda kwenye uchaguzi Raila Odinga.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW