1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Profesa Lipumba afafanua kuhusu milioni 300

Hawa Bihoga27 Machi 2020

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF cha nchini Tanzania, Profesa Ibrahim Lipumba amekiri kuhamishia shilingi milioni 300 kwenye akaunti binafsi kama ilivyotajwa katika ripoti ya CAG na kueleza sababu ya kufanya hivyo.

https://p.dw.com/p/3a7vV
Dar es Salaam Funktionäre der tansanischen Oppositionspartei CUF. Von links: Abbdul Kambaya, Ibrahim Lipumba, Magdalena Sakaya  
Picha: DW/H. Bihoga

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Profesa Ibrahim lipumba amesema kutokana na mgogoro wa kiungozi uliokikumba chama hicho cha siasa, kulikuwa na kila dalili za kuzuiwa kwa akaunti za chama hivyo walihamisha kiasi hicho cha fedha kuelekea katika akaunti ya mwanachama mwaminifu ili kunususru mali hiyo ambayo ilitumika katika maandalizi ya uchaguzi mdogo uliofanyika katika kata takriban 20 Tanzania bara na ubunge wa jimbo la Bimani Zanzibar.

Amesema wakati uchaguzi huo ulipokuwa ukifanyika chama kilikuwa hakipewi ruzuku ya serikali, hivyo walichukua jukumu la kumuandikia msajili wa vyama vya siasa nchini wakiomba fedha ili waweze kushiriki katika uchaguzi, jambo ambalo msajili aliridhia na walipata sehemu ya ruzuku.

Ringen um neue Verfassung in Tansania
Profesa Lipumba akiteta jambo na aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha CUF Maalim Seif Hamad, ambaye amesema mgogoro kati yake na Seif ulisababisha kuhamisha fedha zilizotajwa na CAG.Picha: DW/M.Khelef

Lipumba ameoongeza kuwa hata wakaguzi kutoka katika ofisi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali walipatiwa taarifa na nyaraka za fedha hizo pindi walipofika katika ofisi za chama hicho kwa ajili ya ukaguzi.

Suala hili limeibua mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii huku wengi wakionesha uongozi wa sasa wa chama hicho, umejinufaisha na fedha hizo jambo ambalo limekanushwa vikali na mwenyekiti huyo na kuongeza kuwa hivi sasa wapo kwenye maboresho madhubuti ya mifumo ya fedha ya chama hicho.

Mpango wa kutolewa kwa fedha hizo ulitekelezwa na naibu katibu mkuu bara Magdalena Sakaya, hii ikiwa ni kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.

Mwaka 2016 chama cha CUF kiliingia kwenye mgogoro baada ya mwenyekiti Profesa Lipumba kijuzulu nafasi yake na baadaye kurejea, hatua ambayo ilizushamalumbano ya kiuongozi na hata kupelekea aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekihudumia chama hicho kwa zaidi ya miaka 20 kujiengua na kuondoka na wafuasi waliokuwa wakimuunga mkono.