1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin aishukuru China kwa 'mipango' ya amani ya Ukraine

16 Mei 2024

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema "anaishukuru" Beijing kwa kujaribu kutafuta suluhu la vita vya Ukraine na kupongeza uhusiano unaokuwa wa kiuchumi na China.

https://p.dw.com/p/4futq
Vladimir Putin na Xi Jinping
Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenyeji wake Rais Xi JinpingPicha: Kremlin.ru/REUTERS

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema "anaishukuru" Beijing kwa kujaribu kutafuta suluhu la vita vya Ukraine na kupongeza uhusiano unaokuwa wa kiuchumi na China.

Putin ajiandaa kwa ziara ya siku mbili nchini ChinaAkizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Beijing pamoja na rais wa China Xi Jinping, siku moja baada ya Urusi kusema kuwa wanajeshi wake wanasonga mbele "pande zote" katika uwanja wa vita nchini Ukraine Putin amewashukuru marafiki na

Moscow inasema iko tayari kwa mazungumzo na Ukraine ili kumaliza vita, lakini inasisitiza kuwa Kyiv lazima ikubali sharti la madai ya Urusi kutwaa mikoa ya Donetsk, Kherson, Lugansk na Zaporizhzhia.

Aidha Putin alionekana kukosoa miungano ya usalama inayoongozwa na Magharibi katika eneo la Asia-Pasifiki, na kuitaja kuwa na madhara na "isiyo na tija"  wakati miungano hiyo ikiendelea kuitia wasiwasi Moscow na Beijing.