1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Putin asema Urusi tayari kwa mazungumzo na kuhusu Ukraine

19 Desemba 2024

Rais wa Urusi, Vladimir Putin, amekiri kasoro za vyombo vya usalama vya nchi yake kufuatia mauaji ya Jenerali Igor Kirillov jijini Moscow, yaliyodaiwa kufanywa na Ukraine.

https://p.dw.com/p/4oNC2
Rais wa Urusi Vladmir Putin
Putin asema Urusi tayari kwa mazungumzo na maelewano kuhusu UkrainePicha: Mikhail Tereshchenko/TASS/dpa/picture alliance

Akizungumza katika mkutano wake wa mwisho wa mwaka, Putin amesisitiza haja ya kuboresha mfumo wa ulinzi ili kuepuka makosa makubwa kama hayo. 

Soma pia: Urusi: Jenerali wa ulinzi wa nyuklia Igor Kirillov auawa

Putin pia amesema kuwa Urusi iko tayari kwa mazungumzo na maridhiano kuhusu Ukraine, lakini inahitaji upande wa pili uwe tayari pia. Aidha, alionyesha utayari wa kukutana "wakati wowote" na Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump, ambaye ameahidi kufanikisha mkataba wa amani wa Ukraine mara baada ya kuingia madarakani Januari. 

Putin amebainisha kuwa vikosi vya Urusi vinashikilia udhibiti mkubwa katika vita lakini hajui lini Urusi itarudisha eneo la Kursk lililovamiwa na Ukraine. Kremlin hivi karibuni iliunga mkono ukosoaji wa Trump kwa Biden kuhusu kuiruhusu Kyiv kutumia makombora ya Marekani kushambulia Urusi, hatua inayoongeza mzozo wa karibu miaka mitatu.