Putin: Urusi haikatai kufanya mazungumzo na Ukraine.
30 Julai 2023Matangazo
Hata hivyo, amesema ni vigumu kufanyika kwa mazungumzo hayo, wakati Kyiv ikiendeleza mashambulizi.
Soma zaidi: Putin aipongeza Afrika inavyoshughulikia masuala ya kimataifa
Aidha taarifa nyingine zinasema Saudi Arabia inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mazungumzo ya kusaka suluhu ya amani yatakayofanyika mwishoni mwa wiki ijayo huko Jeddah.
Vyombo kadhaa vya habari vimesema wajumbe kutoka Ukraine, mataifa ya magharibi na mengine yanayoendelea watahudhuria, lakini Urusi haitashiriki.