1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

QUITO : Hali ya hatari nchini Ecuador

16 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFMT

Rais Lucio Gutierrez wa Ecuador ameifuta mahkama kuu ya nchi hiyo katika jaribio la kukomesha mgogoro wa kisiasa.

Pia ametangaza hali ya hatari katika mji mkuu wa Quito kuzima maandamano ya upinzani.Maelfu ya waandamanaji wamekaidi amri hiyo ya hali ya hatari na wamekuwa wakipeperusha bendera,wakivunja vyungu na kutaka Gutierrez ajiuzulu.Hii ni mara ya pili kwa Mahkama Kuu nchini Ecuador kutimuliwa katika kipindi cha miezi minne.

Upinzani unamshutumu Gutierrez kwa kuwa na matendo kama ya dikteta.