SiasaSudan
Washambuliaji wawauwa raia kadhaa wa Sudan
21 Juni 2023Matangazo
Mashuhuda waliozungumza na shirika la habari la Reuters, wamesema wengi ya waliouwawa walikuwa wanakimbia machafuko yanayoukumba mji huo na taifa la Sudan kwa jumla wakilenga kuingia nchi jirani ya Chad.
Washambuliaji huwafyetulia risasi watu wanaotoroka
Kulingana na mashuhuda, makundi ya watu wenye silaha huwavizia na kuwafyetulia risasi watu wanaotoroka mji huo kwa mguu, kuelekea mji wa Adre nchini Chad kiasi kilometa 27 kutoka El Geneina.
Machafuko ya kiasi miezi miwili kwenye mji wa El Geneina yamekuwa yakifanywa zaidi na makundi ya wanamgambo wa makabila ya kiarabu pamoja na wapiganaji wa kikosi chenye nguvu cha RSF kinachopambana na jeshi ya taifa.