Raia wa Australia wanaozuiliwa syria wataka warejeshwe kwao
26 Septemba 2023Kesi inayohusu suala hili ilifunguliwa katika mahakama kuu ya mjini Melbourne takriban mwaka mmoja baada ya Australia kuwarudisha nyumbani kutoka Syria, wanawake wengine wanne na watoto 13 likiwa ni kundi la mwisho la familia za waliokuwa wapiganaji wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu.
Soma pia:Mjumbe wa UN nchini Syria awasihi wafadhili wasisitishe misaada
Shirika la msaada la Save the Children linaloshughulikia suala hilo limesema serikali ya Australia imeshindwa katika jukumu lake la kuwarejesha salama nyumbani raia wake wote kutoka Syria.
Shirika hilo limeiomba mahakama kutowa kibali kinachoonesha raia wa Australia wanazuiliwakinyume cha sheria katika kambi ya Al Roj nchini Syria, na hivyo kuilazimisha serikali kuwarejesha nyumbani watu hao.