1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa wabunge wafanyika Mauritius

10 Novemba 2024

Wananchi wa Mauritius wanapiga kura Jumamosi 10.11.2024 katika uchaguzi wa wabunge. Vituo vya kupigia kura vimeripotiwa kufunguliwa mapema saa moja asubuhi kuruhusu shughuli hiyo kuanza.

https://p.dw.com/p/4mqPI
Uchaguzi wa Mauritius
Mauritius

Polisi wameimarisha ulinzi katika vituo vya kupigia kura wakati upinzani ukionya uwezekano wa kutokea kwa udanganyifu katika taifa hilo linalosifika kwa demokrasia na utulivu.

Uchaguzi huo unafanyika wakati Waziri Mkuu Ravind Kumar Jugnauth na wapinzani wake akiwemo Waziri Mkuu wa zamani Navin Ramgoolan wakiahidi kukabiliana na gharama za maisha katika Kisiwa hicho.

Soma zaidi: Mauritius yatangaza tarehe ya uchaguzi, yavunja Bunge

Kwenye kinyang'anyiro hicho, Chama cha Jugnauth cha Militant Socialist Movement na lliance for Change cha Ramgoolan vinawania viti 62 vya bunge. Jumla ya vyama 68 vinashiriki katika uchaguzi huo. Chama chochote kitakachopata zaidi ya nusu ya viti vya bunge la Mauritius kitakuwa kimeshinda nafasi ya waziri Mkuu.