Raia wa Poland aliyehukumiwa maisha jela Kongo aachiwa huru
28 Mei 2024Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Poland, Radek Sikorski, ameandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa X kuwa raia huyo, Mariusz Majewski, ameachiliwa. Waziri huyo amechapisha video fupi mtandaoni akionyesha wawili hao wakizungumza kwa njia ya simu.
Hata hivyo, hakutoa maelezo ya sehemu alikokuwa mtu huyo.
Majewski mwenye umri wa miaka 52 alizuiliwa na wanajeshi wa Kongo mnamo mwezi Februari na kufikishwa mahakamani kwa shutuma za ujasusi na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.
Wiki iliyopita Rais Andrzej Duda alizungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa Kongo, Felix Tshisekedi, juu ya kuachiliwa huru kwa raia huyo wa Poland.