1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPoland

Raia wa Poland washiriki katika uchaguzi wa bunge

15 Oktoba 2023

Raia nchini Poland leo wanashiriki katika uchaguzi wa bunge utakaoamua uhusiano wa baadaye wa nchi hiyo na Umoja wa Ulaya pamoja na nchi jirani ya Ukraine

https://p.dw.com/p/4XYg0
Waziri mkuu wa Poland Mateusz Morawieck apiga kura yake ya bunge katika uchaguzi wa Oktoba 15,2023 mjini Warsaw
Waziri mkuu wa Poland Mateusz Morawieck apiga kura yake ya bungePicha: Slawomir Kaminski/Agencja Wyborcza/REUTERS

Vituo vya kupigia kura kote nchini humo vilifunguliwa saa kumi na moja alfajiri na vinatarajiwa kufungwa mwendo wa saa moja usiku. Kura ya maoni ya wapiga kura inatarajiwa kufanywa mara tu baada ya zoezi hilo la kupiga kura na matokeo ya mwisho kutangazwa kesho Jumatatu.

Kura ya maoni yakiweka mbele chama cha Nationalist Law and Justice (PiS)

Takriban watu milioni 29 wanaruhusiwa kupiga kura, ikiwa ni pamoja na nusu milioni waliosajiliwa nje ya nchi. Kura za maoni zinaonyesha kuwa chama cha Nationalist Law and Justice (PiS) kitapata kura nyingi zaidi lakini huenda kikatatizika kuunda muungano tawala, na kutoa nafasi kwa upinzani unaoongozwa na mkuu wa zamani wa Umoja wa Ulaya Donald Tusk .