Raia wa Ukraine wanateseka kwa baridi
24 Novemba 2022Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua dhidi ya Urusi kutokana na mashambulizi ya angani dhidi ya miundombinu ya kiraia. Urusi ilirusha mkururo wa makombora kuelekea Ukraine usiku wa kuamkia leo na kuua watu 10, kupelekea kuzimwa kwa mitambo ya nyuklia, kukata usambazaji wa maji na umeme katika maeneo mengi. Hata hivyo hakuna uwezekano wa baraza la usalama kuchukua hatua yoyote katika kujibu ombi la rais wa Ukraine kwasababu Urusi ni mwanachama mwenye kura ya turufu.
Balozi wa Umoja wa mataifa nchini Urusi, Vasily Nebenzya, amejibu akisema ni kinyume na sheria za baraza hilo kwa Zelenskiy kuwasiliana nao na kukataa kile alichokiita "vitisho vya kizembe" kutoka kwa Ukraine na washirika wake katika nchi za Magharibi.