1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Raia wauawa katika mashambulizi ya nchini Urusi na Ukraine

23 Agosti 2023

Raia wameuawa katika mashambulizi nchini Urusi na Ukraine, wakati Moscow ikipigwa na ndege zisizoruka na rubani kwa usiku wa sita mfululizo.

https://p.dw.com/p/4VVmz
Ukraine I Kharkiv
yKombora la Urusi mjini Kharkiv UkrainePicha: Vadym Bielikov/AFP

Raia wameuawa katika mashambulizi nchini Urusi na Ukraine, wakati Moscow ikipigwa na ndege zisizoruka na rubani kwa usiku wa sita mfululizo. Hayo ni wakati vita hivyo vikiingia katika mwezi wake wa 19.

Ukraine, ambayo iliapa kurudisha vita nchini Urusi, imekuwa ikiipiga Moscow na miji mingine ya ndani ya Urusi kwa kutumia mashambulizi ya droni.

Katika mkoa wa Belgorod kwenye mpaka na Ukraine, maafisa wamesema raia watatu waliauawa na askari wa Kyiv leo. Gavana wa mkoa huo Vyacheslav Gladkov amesema askari wa Ukraine walidondosha kilipuzi kutoka kwenye droni na kuwalenga watu mitaani. Urusi na Ukraine zaendelea kushambuliana kwa kutumia droni

Mjini Moscow, shambulizi la droni halikusababisha hasara, baada ya kuanguka kwenye jengo la ghorofa.

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema droni pia zilidunguliwa nje ya mji mkuu Moscow katika wilaya za Mozhaisky na Khimki. Shambulizi hilo la Moscow lilijiri saa chache baada ya Kyiv kusema makombora ya Urusi yalivipiga vijiji viwili karibu na mji wa mashariki mwa Ukraine wa Lyman, na kuwauwa watu watatu na kuwajeruhi wengine wawili.