SiasaAzerbaijan
Rais Aliyev asema Russia ilidungua ndege ya nchi yake
29 Desemba 2024Matangazo
Kiongozi huyo pia ameikosoa Urusi kwa kujaribu "kuficha" ukweli juu ya suala hilo kwa siku kadhaa.
Ameiambia televisheni ya taifa ya Azerbaijan kwamba, amesikitishwa na wakati huo huo kushangazwa na sababu zilizotolewa na maafisa wa Urusi kuhusu chanzo cha ajali hiyo.
Ajali hiyo ya ndege iliyotokea Disemba 25, ilisababisha vifo vya watu 38 kati ya 67 waliokuwemo kwenye ndege hiyo.
Ikulu ya Urusi, Kremlin, ilisema mifumo yake ya ulinzi ya anga ilikuwa ikifyatua makombora karibu na Grozny, mji mkuu wa Chechnya, eneo ambalo ndege hiyo ilijaribu kutua, ili kuzuia shambulio la droni la Ukraine.
Rais wa Urusi Vladimir Putin tayari amemuomba msamaha Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev japo hakukiri moja kwa moja kwamba Moscow ilihusika na ajali hiyo.