Rais Emmanuel Macron kufanya mazingumzo na rais Zelensky
7 Juni 2024Rais Emmanuel Macron leo atamkaribisha katika kasri la Elysee rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ambaye yuko nchini Ufaransa tangu jana alikoshiriki maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 80 tangu vikosi washirika vikiongozwa na Marekani, na Uingereza vilipotuwa katika fukwe za,Normandy, Ufaransa, kuanza operesheni ya kijeshi ya kulikomboa eneo kubwa la kaskazini na Magharibi mwa Ulaya, dhidi ya wanazi wa Ujerumani katika vita vya pili vya dunia.
Kadhalika Zelensky atakutana na rais wa Marekani Joe Biden mjini Paris,ukiwa mkutano wake wa kwanza wa ana kwa ana tangu alipoitembelea Washington mwezi Desemba.
Soma pia:Macron na Scholz wazungumzia mzozo wa Ukraine
Kiongozi huyo wa Ukraine pia atalihutubia bunge la Ufaransa miongoni mwa mambo mengine.
Mwenyeji wake rais Macron amesema, katika ziara hiyo ya Zelensky, amepanga kuzungumzia juu ya suala la uwezekano wa kupeleka wanajeshi wa kutowa mafunzo nchini Ukraine.