1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Rais Joe Biden aziomba SAF na RSF kurejea kwenye mazungumzo

18 Septemba 2024

Rais wa Marekani Joe Biden siku ya Jumanne alizitolea wito pande zinazozozana nchini Sudan "kushiriki tena" kwenye mazungumzo ya amani katika moja ya maoni yake ya moja kwa moja kuhusu mzozo huo.

https://p.dw.com/p/4kjsX
Marekani Washington 2024 | Rais Biden
Rais wa Marekani Joe Biden ameziomba pande zinazopigana nchini Sudan kurejea kwenye meza ya mazungumzo ili kumaliza vitaPicha: Annabelle Gordon/REUTERS

Biden ameziomba pande hizo kurudisha vikosi vyao nyuma ili kuwezesha misaada ya kibinadamu kuwafikia wahitaji bila ya vikwazo.

Amethibitisha kwamba Marekani haitaacha kujitoa kwa ajili ya watu wa Sudan wanaostahili kuwa na uhuru, amani na haki.

Biden aidha alielezea wasiwasi wake juu ya mji wa El-Fasher, moja ya miji mikuu mitano ya jimbo la Darfur, ulio katika mzingiro wa wanamgambo wa RSF tangu mwezi Mei. Mji huo unakaliwa na wakazi karibu milioni 2 waliokimbia makazi yao kutokana na mapigano.

Vita vya Sudan vilianza mwezi Aprili mwaka uliopita kati ya jeshi la Sudan na RSF, na tayari vimesababisha vifo vya maelfu ya watu.