1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan Kusini

Rais Kiir awatimua gavana, wakuu wa jeshi na polisi

10 Desemba 2024

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amemfuta kazi mkuu wa majeshi ya nchi hiyo, mkuu wa polisi na gavana wa benki kuu.

https://p.dw.com/p/4nx9P
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Picha: Samir Bol/ZUMAPRESS/picture alliance

Tangazo lililotolewa jana usiku kwenye televisheni ya umma haikutoa sababu za kufutwa kazi kwa maafisa hao. Lilisema Kiir amemteuwa Paul Nang Majok kuwa mkuu wa majeshi ya ulinzi, akichukua nafasi ya Jenerali Santino Wol.

Mwishoni mwa mwezi Novemba, jaribio la kumkamata aliyekuwa mkuu wa idara ya ujasusi lilizusha makabiliano ya risasi katika mji mkuu Juba. Mapema Oktoba, Kiir alimtimuwa Akol Koor Kuc, ambaye alikuwa mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa tangu nchi hiyo ilipopata uhuru kutoka kwa Sudan mwaka wa 2011.

Alimteuwa mshirika wa karibu kiuchukua nafasi hiyo. James Alic Garang ametangazwa kuwa gavana mpya wa benki kuu, na kumrejesha Johnny Ohisa Damian kwenye wadhifa huo baada ya kumfuta kazi Oktoba 2023. Abraham Peter Manyuat ndiye Inspekta Mkuu wa Polisi akichukua nafasi ya Atem Marol Biar.