1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Macky Sall kutowania muhula wa tatu Senegal

4 Julai 2023

Rais Macky Sall ametangaza kutogombea urais katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2024. Akitowa uwamuzi wake huo amesema Senegal imesheheni viongozi wengine pia walio na uwezo wa kuipeleka mbele nchi.

https://p.dw.com/p/4TNwn
Senegalese President Macky Sall
Picha: Presidency of Senegal / Handout/AA/picture alliance

Tangazo la kiongozi huyo limemaliza minong'ono  iliyokuwa imeenea nchini humo kwamba atatangaza kugombea muhula wa tatu madarakani,hatua ambayo wakosoaji wake wanasema ingekuwa sio halali.

Minong'ono hiyo ilizusha machafuko iliyosababisha umwagaji damu nchini Senegal tangu mwaka 2021 ambapo watu kadhaa waliuwawa, na kuichafua sifa ya nchi hiyo kama ngome ya demokrasia thabiti katika kanda ya Afrika Magharibi.

Jana kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko aliwatolea mwito wafuasi wake kujiandaa kwa maandamano endapo rais Macky Sall angetangaza kugombea urais.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW