1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Mnangagwa apinga madai ya udanganyifu katika uchaguzi

27 Agosti 2023

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa aliyechaguliwa kwa mara nyingine kuiongoza nchi hiyo amewataka wanaohoji matokeo ya uchaguzi wa wiki iliyopita wapeleke malalamiko hayo mahakamani.

https://p.dw.com/p/4Vchc
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa
Rais wa Zimbabwe Emmerson MnangagwaPicha: Jekesai Njikizana/AFP via Getty Images

Mnangagwa ametoa matamshi hayo baada ya kiongozi wa upinzani kusema uchaguzi huo uligubikwa na udanganyifu mkubwa.

Tume ya taifa ya uchaguzi ya Zimbabwe, jana ilimtangaza rais Mnangagwa kushinda kwa asilimia 52.6 ya kura dhidi ya mpinzani wake wa chama cha Citizens Coalition for Change, Nelson Chamisa aliyepata asilimia 44.

Soma zaidi: Rais Emmerson Mnangagwa atangazwa mshindi wa Urais Zimbabwe

Chama cha Mnangagwa cha ZANU-PF kinaendelea kuongoza tangu Zimbabwe ilipopata uhuru  mwaka 1980, chini ya marais wawili ambao ni hayati Robert Mugabe na Emmerson Mnangagwa.