SiasaArgentina
Rais mpya ya Argentina aanza kazi kwa onyo la kukaza mkanda
11 Desemba 2023Matangazo
Javier Milei aliwaambia wafuasi wake mara baada ya kula kiapo siku ya Jumapili (Disemba 10) mjini Buenos Aires kwamba amerithi nchi yenye uchumi mbaya kabisa kutoka kwa mtangulizi wake.
Milei alikiri kwamba serikali yake haina pesa yoyote, lakini aliapa kuchukuwa hatua za haraka kurejesha heshima ya taifa hilo la tatu kwa uchumi mkubwa katika Amerika Kusini.
Soma zaidi: Rais mteule wa Argentina ajadili hali ya uchumi na maafisa wa Marekani
Kiwango cha mfumuko wa bei kimefikia asilimia 140, ambapo asilimia 40 ya raia wanaishi kwenye umasikini.
Milei, anayefuata sera kali za ubepari, anatazamiwa kutekeleza ahadi yake ya kukata matumizi ya serikali, hatua itakayowaathiri mamilioni ya raia waliozowea kupokea ruzuku ya nishati na usafiri.