1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Putin afanya mazungumzo na Rais Lukashenko wa Belarus

Sylvia Mwehozi
23 Julai 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kwamba mashambulizi ya Ukraine ya ulipaji kisasi yameshindwa, wakati alipoanza mazungumzo ya siku mbili na mwenzake wa Belarus na mshirika wa karibu Rais Alexander Lukashenko.

https://p.dw.com/p/4UHmZ
St. Petersburg | Putin akutana na Alexander Lukaschenko
Rais wa Urusi Vladimir Putin na Alexander LukaschenkoPicha: Alexander Demianchuk/TASS/dpa/picture alliance

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kwamba mashambulizi ya Ukraine ya ulipaji kisasi yameshindwa, wakati alipoanza mazungumzo ya siku mbili na mwenzake wa Belarus na mshirika wa karibu Rais Alexander Lukashenko. Video iliyochapishwa mapema leo na kitengo cha habari cha Lukashenko iliwaonesha viongozi hao wakiwasili katika kasri la Konstanti-novsky la mjini St. Petersburg kabla ya mazungumzo yao kuanza.

Viongozi hao wa muda mrefu walikutana kwa mara ya kwanza tangu Lukashenko asaidie kumaliza uasi wa mamluki wa Urusi Wagner nchini Urusi mwezi uliopita, katika kitisho kikubwa zaidi kwa utawala wa Putin wa zaidi ya miongo miwili.

Kwenye mazungumzo hayo, yatakayodumu kwa muda wa siku mbili, wawili hao watazungumzia masuala ya usalama mashariki mwa Ulaya. Urusi na Belarus ni washirika wa muda mrefu katika uhusiano ambao Moscow ndiyo inayotawala sehemu kubwa ya ushirika huo.