Rais Putin atumai kutakuwa na suluhisho la amani Karabakh
20 Septemba 2023Bila ya kutaja makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa mapema leo, Putin amesema alipokutana na waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi kwamba wanawasiliana kwa karibu na pande zote zinazovutana.
"Walinzi wetu wa amani wanashirikiana kwa karibu na pande zinazohusika na mzozo huu. Wanafanya kila liwezekanalo kuwalinda raia wapatao 2,000, miongoni mwao wakiwemo watoto 1,000. Ninarudia tena, tuna mawasiliano ya karibu na pande zote na mamlaka za Yerevan, Stepnakert na Baku. Ninatumaini tutafanikiwa kumaliza mapigano na kusuluhisha suala hili kwa njia ya amani,"amesema Putin.
Muda mfupi baada ya makubaliano hayo, Arzebaijan imesema itafungua njia salama kwa vikiso vilivyojitenga vya Armenia kama sehemu ya makubaliano hayo na kusema shughuli zote zinaratibiwa na walinda amani wa Urusi.
Soma pia: Nagorno-Karabakh: Azerbaijan yathibitisha usitishaji mapigano