1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Samia aendelea na ziara yake Lindi

18 Septemba 2023

Akiwa ziarani, Rais huyo ameonesha kukerwa na mambo mbalimbali yanaoendelea ikiwemo udhaifu wa kimahusiano uliopo baina ya viongozi ambao ni watendaji wa serikali.

https://p.dw.com/p/4WUTA
Samia  amesema serikali inatarajia kujenga kiwanda cha ukubwa wa kati cha kubangua korosho
Samia amesema serikali inatarajia kujenga kiwanda cha ukubwa wa kati cha kubangua koroshoPicha: Presidential Press Service Tanzania

Akiwa mkoani Lindi amezungumzia changamoto ya migogoro ya wakulima na wafugaji na athari za wanyama waharibifu, huku akisema ni miongoni mwa mambo yatakayoshughulikiwa na serikali kuu kutokana nah atua mbalimbali za wilaya na mkoa kushindwa kufua dafu juu ya changamoto hizo, huku akionesha kusikitishwa kwake na hatua ya wananchi 10 kuuawa na tembo katika kipindi cha mwaka 2021 hadi 2023.

 Aidha Rais Samia amebaini unyonywaji wa wakulima kupitia watendaji katika vyama vya wakulima, ambao wamekuwa wakianzisha tozo na makato kwenye mazao ambayo haitambuliki kisheria, haikaguliwi, na taarifa zake hazirudishwi kwa wananchi.
Kadhalika ameonya juu ya mila na desturi kandamizi zinazofanywa kwa watoto wa kike zinazopelekea kuwakosesha nafasi ya kupata elimu na kumwataka wazazi na walezi kutumia pesa wanazozipata kwenye  mavuno kupitia mazao mbalimbali kukuza uchumi wa vipato vyao badala ya kuendekeza mila hizo.

Uwekezaji wa bandari ya Mtwara

Rais Samia na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Rais Samia na Waziri Mkuu Kassim MajaliwaPicha: Presidential Press Service Tanzania

Hata hivyo, Rais Samia ameagiza kutumika kwa bandari ya Mtwara katika shughuli za usafirishaji kufungua uchumi wa mikoa ya kusini kupitia uwekezaji wa bandari ambao umetumia zaidi ya billion 157.8 za Kitanzania katika kusafirisha Korosho ghafi na bidhaa zingine katika nchi za kusini mwa Afrika kama Malawi, Msumbiji na Zambia, amezunguzia hatua ya ujenzi wa mradi mkubwa wa kuchakata gesi asilia LNG unojengwa katika Mkoa wa Lindi unaogharimu Dola bilioni 30, ambao unatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 10000 kwa watanzania Pamoja na ujenzi wa Barabara za kiuchumi na ugunduzi wa madini,

Rais Samia anaendelea na ziara katika mkoa wa Lindi, na ziara hii inafanyika katika mikoa ya Kusini baada ya kipindi cha zaidi ya miaka mitano ambapo hajawahi kufika kiongozi wa juu kwani mara ya mwisho ilikuwa 2019, April 2- 4, ambapo Hayati John Pombe Magufuli alifanya ziara katika mikoa hii.