Rais Tshisekedi aidhinisha dola mil. 10 kukabiliana na mpox
23 Agosti 2024Matangazo
Kongo imeripoti zaidi ya visa vipya 1,000 vya ugonjwa wa Mpox katika kipindi cha wiki moja iliyopita. Mamlaka za afya za Afrika zimeomba chanjo zinazohitajika kwa haraka kusaidia kupambana na tishio la Mpox linaloongezeka katika bara hilo.
Wakati huo huo Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO, limesema washirika wake kama vile Gavi na Unicef wanaweza kuanza kununua chanjo ya mpox kabla ya kuidhinishwa na Umoja wa Mataifa.
Hatua hiyo inakusudia kuharakisha chanjo hiyo barani Afrika kupambana na mlipuko wa Mpox. Baadhi ya chanjo za Mpox zilizotolewa zinatarajiwa kuwasili Afrika wiki ijayo.