1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBelarus

Rais wa Belarus aelekea China kwa ziara ya pili mwaka huu

3 Desemba 2023

Rais wa Belarus Alexander Lukashenko anaelekea China leo kwa mazungumzo na kiongozi wa nchi hiyo Xi Jinping. Hayo yameripotiwa na shirika la habari la serikali ya Belarus

https://p.dw.com/p/4ZioB
Rais wa Belarus Alexander Lukashenko akizungumza na wanahabari wa kigeni mjini Minsk mnamo Julai 6,2023
Rais wa Belarus Alexander LukashenkoPicha: Alexander Zemlianichenko/AP/picture alliance

Lukashenko, ambaye kwa mujibu wa shirika la habari la China BelTA, alikaribishwa kwa heshima zote kijeshi alipoitembelea China mnamo Februari 28 hadi Machi 2, wakati huu anakwenda kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Belta imenukuu kitengo cha habari cha Lukashenko kikisema kuwa mazungumzo kati ya viongozi hao wawili yatafanyika mjini Beijing.

Masuala yatakayojadiliwa wakati wa mkutano wa Lukashenko na Xi

Agenda ya mkutano huo inajumuisha masuala ya kiuchumi, biashara, uwekezaji na ushirikiano wa kimataifa.

Baada ya mazungumzo yao ya kwanza mwaka huu, Xi alisema kuwa ushirikiano kati ya China na Belarus hauwezi kuvunjika na kwamba pande hizo mbili zinapaswa mara kwa mara kuimarisha uaminifu wa kisiasa na kubaki kuwa washirika wa kweli.