Rais wa Iran autetea mkataba wa nyuklia
9 Juni 2021Matangazo
Katika mjadala huo wa pili wa wagombea urais, wagombea wenye msimamo mkali kwa mara nyingine waliyabeza matumaini ya utawala wa Rouhani kuhusu mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 na mataifa yenye nguvu duniani ambao unasuasua.
Rouhani aliyeonekana mwenye hasira alitoa matamshi hayo yaliyowalenga wakosoaji wake, kupitia hotuba yake kwa baraza la mawaziri iliyorushwa kwenye televisheni.
soma zaidi: IAEA yataka majibu kutoka Iran kuhusu shughuli za nyuklia
Amesema wanasiasa wenye misimamo mikali, ambao kwa muda mrefu wanayakosoa makubaliano hayo wanatakiwa kuchunguzwa kuhusiana na iwapo wanataka nafuu ya vikwazo kwa kurejea kwenye makubaliano hayo yaliyozorota baada ya Donald Trump kujiondoa mwaka 2018.