Rais wa Israel alaani mashambulizi mjini Amsterdam
8 Novemba 2024Rais wa Israel Isaac Herzog, leo amelaani mashambulizi mjini Amsterdam nchini Uholanzi baada ya machafuko kuibuka kati ya waandamanaji wanaoiunga mkono Palestina na mashabiki wa klabu ya Maccabi Tel Aviv mjini Amsterdam.
Katika taarifa katika mtandao wa X, Herzog amesema mashambulizi hayo yanaibua kumbukumbu ya mashambulizi yaliyofanywa na kundi la Hamas mwaka jana pamoja na mashambulizi ya chuki dhidi ya Wayahudi wa Ulaya katika karne zilizopita.
Soma: Maandamano ya kumtaka Benjamin Netanyahu ajiuzulu yafanyika Tel Aviv
Kwa upande wake, waziri mkuu wa Uholanzi Dick Schoof amesema:
"Picha na ripoti tunazosikia ni za kusthua na kulaaniwa kabisaa. Nadhani hatua zote zinapaswa kuchukuliwa kuwasaka na kuwashtaki wahusika. Huu ni unyanyasaji wa chuki dhidi ya Wayahudi. Kwamba hii inaweza kutokea mwaka wa 2024 inakosa maelezo na imevuka mipaka kabisa''.
Waziri Mkuu wa zamani wa Israel Naftali Bennet amelizungumzia tukio hilo na kuyataja kuwa mauaji ya kimbari yanayoendelea.